
Awali Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa alimkabidhi kijana huyo shilingi milioni moja kama zawadi kutokana na Ujasiri wake katika tukio hilo
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila akitoa ya ajali hiyo wakati wa kuaga miili ya waliofariki amesema kuwa waliofariki ni 19 na waliookolewa ni watu 26
Amesema kuwa Abiria waliokuwa kwenye ndege hiyo ni 43 ambapo wasafiri walikuwa 39
"Ndege ile ilikuwa na abiria 43, katika hao 39 ni wasafiri, wawili ni wahudumu na wawili mmoja ni rubani na mmoja ni msaidizi wake"
"Waliofariki ni 19 na waliookolewa katika ajali waliokuwa wasafiri ni 24 na sio 26 kama ambavyo tuliripoti jana"
"Kijana mmoja aliyejitupa ndani ya maji na ndiye aliyechukua ile kasia na kufungua ule mlango, kwa bahati mbaya na yeye aliumia akazirai na wenzake wakamuokoa na alipofika hospitali walimjumuisha kuwa ni watu waliokuwa ni wasafiri, anaendelea vizuri sasa" amesema Chalamila na kuongeza kuwa mmoja aliyekuwa amejumuishwa katika majeruhi ni mhudumu wa uwanja wa ndege ambaye alipata mshtuko na kupelekwa hospitalini
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa gharama za mazishi ya waliofariki yote yatagharamiwa na serikali ya Tanzania