Jumatano , 20th Feb , 2019

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shana amewaaga maofisa wa polisi na waandishi wa habari mkoani Mwanza kwa namna ya tofauti baada ya nafasi yake kuteuliwa Kamanda Jumanne Muliro ambaye alikuwa Kindondoni Jijini Dar es salaam.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Simon Sirro.

Akizungumzia na baadhi ya maaskari polisi mkoani Mwanza huku akionekana na mtu mwenye furaha Kamanda Shana amewataka polisi kumpa ushirikiano kamanda huyo mpya.

Akizungumza kwa sauti ya ujazo na kuyataja kwa madaha baadhi ya maneno, Kamanda Shana amesema, "katika mabadiliko yalioyofanyika hivi karibuni aliteuliwa Kamanda Jumane Muliro  kushika kamanda wa polisi Mwanza."

"Niwaombe kwa dhati kama mlivyonipa mimi ushirikiano kwa jiji la Mwanza nyinyi mnaloliita Rock city na mimi naliita the beatifully city of Mwanza liendelea kuwa shwari."

"Nashukuru katika kipindi changu sikuwahi kulalamikiwa na chama chochote cha siasa, tulifanya kwa ushirikiano niwaalike vyama vingine vije vijifunze Mwanza  juu ya kulinda amani. shangilia vyama vya siasa machampioni wa amani", ameongeza Kamanda Shana.

Oktoba mwaka jana akiwa wilayani Butiama kwenye kumbukumbu ya siku ya Mwalimu Julius Nyerere Kamanda Shana alizua mjadala kwenye mitandao ya kijamii wakati akiwasalimia baadhi ya wananchi wilayani humo ambapo alitumia salama ya Chama Cha Mapinduzi.