Jumamosi , 23rd Mar , 2019

Mwanamitindo wa Tanzania Flaviana Matata, ameomba msaada wa namna atakavyoweza kumsaidia kijana ambaye anatamani kujiua kutokana na ugumu wa maisha.

Flaviana Matata

Flaviana amefikia hatua ya kuomba msaada baada ya mfuasi mmoja kwenye mtandao wa Instagram, kumuandikia hivyo hata baada ya kumshauri ameendelea kusisitiza jambo hilo.

Flaviana amesema kwamba hamfahamu mtu huyo ingawa anaogopa kutokana na tukio hilo.

"Kuna mtu kaniandikia Instagram anatamani kujiua sababu ya ugumu wa maisha. I don’t know this person ila naogopa na bahati mbaya i cant help kila anayeniomba msaada. I tried to talk some senses to him ila bado, where do we report such people in Tanzania??! Help please" Matata.