Ijumaa , 24th Jan , 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amesema Ndege za Tanzania zinatarajiwa kuanza safari za moja kwa moja kuelekea nchini China

Rais Magufuli

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye mkutano na viongozi wa CCM na Jumuiya zake ambapo bado kuna mpango kuagiza Ndege nyingine.

Rais Magufuli amesema kuwa "nani alitegemea nchi iwe na Ndege, mwezi unaokuja tunaanza safari za Ndege kutoka hapa hadi china moja kwa moja, Ndege nyingine zinakuja na tumenunua Cash, tajiri huwezi nunua kwa kukopa"

"Idadi ya Watalii wameongezeka kutoka Mil. 1.1 mwaka jana hadi zaidi ya Mil. 1.5, tunataka tujenge uchumi wa nchi iliyo tofauti, lakini hata kuzaana hatuko nyuma, kuzaa ni uchumi msidanganywe"