Jumapili , 6th Oct , 2019

Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), imesitisha safari za ndege zake zinazofanya safari kuelekea Afrika Kusini, kuanzia kesho Oktoba 7 na kuagiza abiria wote waliokuwa wamekata tiketi kurudishiwa nauli zao.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa ATCL Ladislaus Matindi, na kuagiza mawakala wote kurejesha nauli za abiria, waliokuwa wamekwishakata tiketi kwa ajili ya safari na kwamba safari hizo zimesimamishwa hadi taarifa kamili itakapotolewa tena.

Ikumbukwe kuwa hapo awali, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, alitoa tamko rasmi la kusitisha safari za ndege hizo kufuatia vuguvugu la machafuko lililokuwa likiendelea Afrika Kusini, kati ya wazawa na raia wa mataifa mengine.

Mnamo Agosti 23, 2019,ndege ya ATCL aina ya Bombadier Q220 - 300, ilishikiliwa nchini humo kwa amri ya mahakama ya Guateng nchini humo, ambapo baadaye iliachiwa huru baada ya mawakili wa Serikali kuishinda kesi dhidi ya mkulima.