Audio: Waliompiga risasi Lissu kusomewa 'Albadili'

Thursday , 14th Sep , 2017

Baraza la vijana wa CHADEMA wilayani Muheza Mkoani Tanga, wamethibitisha kutaka kusoma albadili ili kumjua mtu aliyempiga risasi mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Akizungumza na mwandishi wa habari wa East Africa Television mwenyekiti wa BAVICHA wilaya ya Muheza Mkoani Tanga bwana Joseph Saja amesema wameona ni vema kufanya hivyo ili kuisaidia serikali kuweza kuwatambua watu wasiofahamika, ambao wameweka rehani maisha ya Mwanasheria mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu.

Bwana Saja amesema albadili hiyo haina lengo la kumdhuru mtu, isipokuwa wawatambue watu hao na kuwashikisha adabu, ili iwe somo kwa wengine na vitendo hivyo visiendelee kufanyika.

Msikilize hapa chini