Alhamisi , 4th Jun , 2020

Baada ya CHADEMA, kuwataka watangaza nia ya kugombea nafasi ya Urais ndani ya chama hicho wajitokeze, NCCR Mageuzi nao wamesema kuwa wanatarajia kutoa ratiba ya uteuzi wa wagombea Urais, Ubunge na Madiwani juma lijalo, na kuiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutenda haki katika uchaguzi ujao.

Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia.

Hayo yamebainishwa leo Juni 4, 2020, na Mwenyekiti wa chama hicho James Mbatia, Jijini Dodoma na kusema kuwa kwa sasa kimefungua milango kwa vyama vingine vya siasa nchini, ambavyo vipo tayari kushirikiana ili kuiondoa Serikali ya Chama cha Mapinduzi madarakani.

Aidha Mbatia amezungumzia kuhusu mlipuko wa Virusi vya Corona na kuwaomba wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zaidi.