Baada ya kutoka gerezani Mbowe akutana na jingine

Alhamisi , 14th Mar , 2019

Wamiliki 34 wa viwanja katika eneo la maendelezo ya viwanda la Weruweru katika Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro akiwemo Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe wako ‘njia panda kufuatia kudaiwa kodi ya pango la ardhi.

Freeman Mbowe.

Mbowe na walimiki wengine wako njia panda, baada ya Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya kutangaza hatua zilizochukuliwa mpaka sasa kuwa ni pamoja na ilani ya ubatilisho wa umiliki wao kutumwa kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.

Akitangaza orodha hiyo, wakati wa mkutano wa siku mbili wa kusikiliza kero, malalamiko na migogoro ya ardhi, Sabaya amesema watu hao wamo katika orodha ndefu ya wamiliki ambao viwanja vyao vimeombewa kibali cha kufutwa.Freeman Mbowe akizungumza

"Huko nyuma watu walipewa viwanja mashine tools, viwanja 52 vikubwa wakaambiwa waendeleze kwa sababu ni eneo la viwanda, wana miaka mingapi?. Unapewa shamba (eneo la kiwanja) mwaka 1984, kabla mimi sijazaliwa, hajawahi kufanya lolote", amesema Sabaya.Mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya

"Sasa Afisa Ardhi ameshaandika barua ya kubatilisha hivyo viwanja, niwaambie hapa hapa wako watu mnaowaheshimu na hawalipi kodi na leo ntawataja humu", ameongeza Sabaya.

Jumla ya kiasi ambacho Mbowe na wenzake wanadaiwa

Idadi hiyo ya watu 34, inafanya jumla ya kiasi cha fedha kinachodaiwa kutokana na pango la ardhi kufikia Shilingi 1, 828, 166, 096.

Mbali na Mbowe wamo pia Mkuu wa mkoa wa zamani wa Kilimanjaro, Cynthia Hilda Ngoye, Kiwanda cha Kutengeneza Vipuri cha Kilimanjaro Mashine Tools Manufacturing Company Ltd kilichopo chini ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) na wafanyabiashara maarufu wa mji wa Moshi wanaomiliki shule binafsi na makampuni ya utalii.