Jumatatu , 20th Mei , 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemuapisha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada baada ya kumteua mwezi Januari mwaka huu.

Rais Magufuli akimuapisha Dkt. Mpoki Ulisubisya

Dkt. Mpoki Ulisubisya alikuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ambaye huenda akakumbukwa sana na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kufuatia kuwa miongoni mwa Madaktari wa mwanzo ambao walimpatia huduma ya kwanza alipopigwa risasi Septemba 7, 2017.

Hafla ya kumuapisha kiongozi huyo imefanyika Ikulu jijini Dar es salaam, ambapo baada ya kuapishwa  anatarajiwa kusafiri mara moja kwa ajili ya kuelekea eneo lake la kazi nchini Canada.

Januari 8, 2019 Rais Magufuli Dkt. Zainabu Chaula kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (anayeshughulikia afya), ambapo kabla ya uteuzi huo Dkt. Chaula alikuwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI.