Ijumaa , 21st Feb , 2020

Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), limetoa tafsiri ya Lugha Fasaha ya Kiswahili juu ya maana ya neno Kigogo na kusema lina maana zaidi ya moja ikiwa ni pamoja na kuwa ni kipande kizito cha mti kilichokatwa, huku maana nyingine ikieleza kuwa ni mtu mwenye cheo kikubwa.

Pichani Kigogo wa Twitter na Nembo ya BAKITA.

Akijibu swali lililohoji sababu ya mtu anayejiita Kigogo katika mtandao wa Twitter, kutumia jina hilo, leo Februari 20,2020 aliloulizwa na EATV &EA Radio Digital, Mchunguzi wa lugha kutoka BAKITA Mussa Kaoneka, amesema huenda mtu huyo alifanya hivyo kulingana na taarifa zake anazoziandika.

"Kigogo ni kipande cha mti kilichokatwa kutoka kwenye mti mkubwa, nyingine ni mtu mwenye madaraka kwenye Serikali ama taasisi binafsi, huyo wa Twitter nahisi ametumia uficho tu ili asijulikane ni nani, pia ni mtu ambaye anadai anaweza kupata taarifa za watu mbalimbali" amesema Kaoneka.