Jumatatu , 20th Jan , 2020

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Bashiru Ally, amesema moja ya mambo makubwa aliyoyafanya Rais Magufuli, ni kurejesha matumaini mapya kwa wanyonge ndani ya Tanzania.

Rais Magufui na Katib u Mkuu wa CCM Bashiru Ally

Bashiru ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanachama wa chama hicho mkoani Kigoma. 

"Moja ya mambo ambayo hayatasahaulika kwa awamu ya Tano ni kurejesha matumaini mapya ambao ni wanyonge, ambao waliwahi kukata tamaa".

"Kwa hiyo mkiulizwa ni jambo gani jipya limefanyika kwa kipindi cha awamu ya tano na kupimika na kuonekana kila mahala, waelezeni jambo jipya ni matumaini mapya kwa wanyonge" amesema Dkt Bashiru.