Alhamisi , 26th Jan , 2023

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Adam Malima amezindua  ujenzi wa Vivuko vitatu vyenye thamani ya Tsh. Bil 15.6, ujenzi unaotarajiwa kukamilika mwezi Julai mwaka huu

Akizingumza wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa mradi huo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima amewataka wasimamizi wa mradi huo ambao ni kampuni ya Songoro Marine kukamilisha mradi huo kwa wakati na katika viwango vinavyotakiwa

Kwa upande wake Mbunge wa Buchosa Erick Shigongo na Mbunge wa Ukerewe Joseph Mkundi wamesema vivuko hivyo vitasaidia kitatua adha ya usafiri kwa wananchi wa Maeneo yao

Naye mkurugenzi wa kampuni ya Songoro Marine Ltd inayojenga Mradi huo, Eng. Meja Songoro akaishukuru Serikali kwa kuamini kampuni za ndani ya Tanzania na kuwahakikishia kukamilisha kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa.