
Hayo yamebainishwa kwenye ukurasa wa 175 wa Kitabu cha hotuba ya makadirio ya bajeti Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka ujao ambayo iliwasilishwa Bungeni mapema wiki hii na Waziri Philip Mpango, ambapo imebainishwa kuwa kwa 2019/2020, ofisi ya Taifa ya Ukaguzi inatarajiwa kutumia jumla ya bilioni 61.3.
Kati ya hizo ni shilingi bilioni 55, ni matumizi ya kawaida na matumizi ya mengineyo shilingi bilioni 40 na shilingi 6.3 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Makadirio hayo yaliwasilishwa bungeni jijini Dodoma Jumatatu na Waziri wa Fedha na Mipango na kuidhinishwa na Bunge.
Akizungumza wakati wa kuwasilisha hotuba ya bajeti jijini Dodoma Waziri Mpango, amesema kuwa katika mwaka ujao wa fedha ofisi ya CAG itaendelea kuimarisha ukaguzi wa mapato na matumizi ya serikali kwa ajili kuimarisha uwajibikaji na uwazi kwenye matumizi ya rasilimali umma.