Jumatatu , 19th Mar , 2018

Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza, Juma Sweda ameivunja bodi ya chama cha kuweka na kukopa fedha kwa vijana wilayani humo baada ya kugundulika watumishi 25 na wajumbe kujipatia jumla ya fedha Milioni 17 kinyume na utaratibu.

Bw. Sweda amefanya maamuzi hayo kufuatia watumishi hao kujiunga kwenye chama hicho bila kuwa na sifa pamoja na kushindwa kurejesha fedha walizokopa tangu mwaka 2014 na kuagiza Jeshi la Polisi wilayani Misungwi mkoani humo kuwakamata.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa ili kukinusuru chama hicho ameivunja bodi hiyo ili kuweza kupata viongozi watakaokuwa na sifa lakini pia na wanachama wenye sifa ya kuwa vijana.

Msikilize hapa chini Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Juma Sweda.