Bomba la gesi kutoka Mtwara lawaka moto

Jumanne , 9th Jan , 2018

Moto mkubwa unawaka eneo la Buguruni kwa Mnyamani baada ya mafundi wa Dawasco kutoboa bomba la gesi kutoka Mtwara kimakosa, na kuleta madhara kwa nyumba za jirani.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum jijini Dar es salaam, Benedict Kitalika, na kusema kwamba mafundi hao walikuwa wakichimba kwa ajili ya kupitisha mabomba yao, na ndipo wakatoboa bomba hilo kimakosa.

Kamanda Kitalika ameendelea kwa kusema kwamba wameshawasiliana na watu wa Mtwara na kufunga bomba hilo, ili kupunguza kasi ya gesi, na kufanikiwa kwani mpaka sasa kasi ya moto imeanza kupungua.

Kamanda Kitalika amesema mpaka sasa hakuna taarifa ya kifo au majeruhi yeyeote, lakini kumeripotiwa kuwa nyumba za maeneo ya jirani zimeshika moto huo lakini kikosi cha zimamoto kinaendelea na jitihada za kuzima.

Msikilize hapa chini