Ijumaa , 22nd Jun , 2018

Mbunge wa CCM, Abdallah Bulembo ameihoji serikali kuwa ni lini wananchi wa  Makoko huko Musoma watalipwa stahiki zao za toka 1982 ambazo wanastahili kulipwa baada ya kuachia maeneo yao.

Mbunge wa CCM, Abdallah Bulembo

Mh. Bulembo amehoji kwamba mpaka leo ni miaka 36 imekwishapita na wananchi hao bado hawajalipwa haki yao ya Bilioni 1.4, hivyo Serikali inatoa tamko gani kwa wananchi  hao?

Akijibu swali hilo Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amesema kuwa kutokana na kuwa Bulembo amesemea swala mahsusi linalohsisha fidia basi atalichukua jambo hilo na kwenda kujua Status yake ili kufahamu kama tathmini zilikwishafanyika na kama fedha hizo zinastahili kulipwa.