Jumatano , 11th Jul , 2018

Mbunge wa jimbo la Kilwa Kusini (CUF), Selemani Bungara ‘Bwege’ amesema kuwa vyama vya upinzani vinapaswa kushikamana kwa ajili ya mafanikio katika uchaguzi wowote utakaofanyika nchini.

Mbunge wa jimbo la Kilwa Kusini (CUF), Selemani Bungara ‘Bwege'

Akizungumza kupitia KIKAANGONI ya East Africa Television inayorushwa kupitia ukurasa wake wa facebook, Bwege amesema hakuna chama cha upinzani kitakachoweza kukiondoa chama tawala ‘ chama cha mapinduzi ’ madarakani bila ya mshikamano na vyama vingine vya upinzani.

“Migogoro mingi katika vyama vya upinzani hasa CUF haitaleta tija ya kukiondoa Chama Cha Mapinduzi (CCM) madarakani iwe ni kwenye majimbo au katika uchaguzi wa Rais, kinachoitajika ni mshikamano baina ya vyama vya upinzani” ,amesema Bwege.

Aidha Bwege ameongeza kuwa migogoro mingi ndani ya CUF na itikadi zilizojengwa na watu wengine kutoka nje ya CUF kwamba chama hicho kimejengwa zaidi na itikadi ya dini ya kiisiramu na kutokana na uvumi huo wakiristu wengi walihama chama hicho.