Ijumaa , 12th Apr , 2019

Mbunge wa Kibamba (CHADEMA), John Mnyika amehoji ni kwanini Wabunge hawajapatiwa ripoti ya uchunguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kama kanuni za Bunge zinavyosema.

Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali CAG, Prof Assad

Mbunge Mnyika amehoji hayo bungeni jijini Dodoma alipoomba mwongozo wa kiti cha Spika ambapo amesema kitendo cha Wabunge kutogawiwa ripoti hiyo hakiungwi mkono na Wabunge.

Baada ya kauli hiyo Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge akasema ripoti hizo za CAG haziwezi kugawiwa kwa wabunge kama Mnyika anavyotaka kwa kuwa kanuni haziruhusu kufanya hivyo.

Mwenyekiti wa Bunge Andrew Chenge amesema, "kanuni inasema taarifa ya CAG, iwasilishwe bungeni haijaandikwa ni lazima igawiwe kwa Wabunge"

Aprili 10, 2019 Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali CAG, alizungumza na waandishi wa habari ambapo alitoa hadharani ripoti yake ya ukaguzi ambapo alibainisha kasoro mbalimbali kwenye taasisi za umma.