Jumamosi , 24th Sep , 2022

Katibu wa Baraza la wanawake wa Chadema nchini (BAWACHA) Catherine Ruge amekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mara katika ukumbi wa Musoma club Halamashauri ya Musoma Muda mfupi kabla ya kufanya Mahojiano na Waandishi wa habari juu ya mauaji ya watu watatu wanaodaiwa ni Majambazi .

 

Mauaji hayo ya watu wa tatu yalitokeaa siku ya semptemba 22 katika wilaya ya Serengeti ambambo moja ya waliouwawa ni mjomba wake na katibu hiyo wa chadema anaefahamika kwa jina la Mugare Makori.

Chanzo cha kukamatwa kwa Catherine Ruge ni kwa ajili ya mahojiano na Jeshi la polisi ili kuelezea  mauaji ya watu hao wa tatu .

Akithibitisha kukamatwa kwa katibu hiyo wa BAWACHA,  kamanda wa Jeshi la Polisi  Longinus Tibishibwamu amesema wamemkamata Ruge kwani ni takwa  la kisheria ambapo anatakiwa kuthibitisha tuhuma za Jeshi la Polisi  kufuatia mauaji ya watu watatu waliouawa wakati wakirushiana risasi na sskari polisi.