Jumamosi , 16th Dec , 2017

Kamati Kuu ya Halmashauri  Kuu  ya  Taifa  ya  CCM,  na  kwa  niaba  ya  Halmashauri Kuu  ya  Taifa  (NEC) imefanya  uteuzi  wa  mwisho  kwa  wanachama wa  CCMwatakagombea  katika  Uchaguzi wa Ubunge katika Majimbo matatu.

Katibu Mwenezi wa NEC-Itikadi na uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesema kwamba katika kikao hicho kilichofanyika jana mjini Dodoma chini ya mwenyekiti wa chama cha CCM ambaye pia ni Rais , Dkt. John Pombe Magufuli  kilipitia majina ya walio omba dhamana na kwa kuzingatia misingi ya maadili, uchapakazi, uwakilishi   bora na wenye tija kwa wananchi.

Taarifa hiyo imesema kamati kuu imewateuwa  Monko  Justine  Joseph,  Mgombea  wa  CCM Jimbo la Singida Kaskazini,Ndg.  Damas  Daniel  Ndumbaro,  Mgombea  wa CCM Jimbo la Songea Mjini na Ndg.  Dkt.  Stephen  Lemomo  Kiruswa,  Mgombea wa CCM Jimbo la Longido.