Ijumaa , 19th Jul , 2019

Chama cha mapinduzi CCM kimetoa onyo kwa baadhi ya viongozi watakaotumika kuingiza mamuruki ya watu, ili kugombea nafasi katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwishoni mwa mwaka huu nchini kote.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa Humfrey Polepole.

Akiwa katika ziara ya siku moja mkoani Iringa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa Humfrey Polepole, amekemea vikali vitendo ambavyo vinatajwa kuwa mwiba kwa chama hicho na kusababisha kushindwa katika chaguzi jambo ambalo amesema halivumiliki.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Iringa Dtk Abel Nyamahanga amewataka wanachama na viongozi wa chama hicho, kushikamana ili kuibuka na ushindi katika chaguzi zijazo ikiwemo uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2020.

Ziara ya Polepole imelenga kuwajengea uwezo viongozi wa mitaa wakiwemo wenyeviti wa mitaa, Mabalozi na makatibu kata wa chama hicho katika Manispaa ya Iringa, ili kujiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa.
 

Zaidi Tazama Video hapa chini