Jumatano , 20th Mar , 2019

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Zuberi Kabwe, amesema kwamba wapo hadi watanzania waliopo Chama Cha Mapinduzi wameanza kuulizia namna ya kujiunga na chama cha ACT- Wazalendo.

Zitto Kabwe

Zitto ameyathibitisha hayo ikiwa ni siku moja tu tangu alipomkabidhi aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif, baada ya kushindwa kesi Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam iliyohalalisha uongozi wa Lipumba ndani ya CUF.

"Nawathibitishia Watanzania kuwa hata wanaotaka mabadiliko kutoka ndani ya CCM   waliochoshwa na kuburuzwa wameanza kutufuata kuulizia lini na vipi wanaweza kujiunga na ACT Wazalendo", amesema Zitto.

Mbali na hayo Zitto amefafanua kwamba maamuzi ya Maaalim Seif kuingia ACT halikuwa jambo la kukurupuka na kwamba ulikuwa mchakato wa muda mrefu.

"Muziki huu ni mkubwa na wala watu wasidhani maamuzi na maandalizi yake yalianza juzi baada ya hukumu ya Mahakama. Ni kazi ya miaka 3 ya kutafuta njia bora ya kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini kwetu. Watanzania watashangaa", amaeongeza Zitto.