Jumamosi , 15th Feb , 2020

Mbunge wa Ndanda CHADEMA Cecil Mwambe ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge na nafasi za uongozi ndani ya CHADEMA na kuomba kujiunga Chama Cha Mapinduzi.

Mbunge wa Ndanda CHADEMA Cecil Mwambe

Mwambe amefikia uamuzi huo leo Februari 15, 2020 katika makao makuu ya CCM Lumumba, jijini Dar es salaam ambapo amedai sababu ya kufanya hivyo ni kutokana na kuwepo kwa makundi ya cama hicho.

'Kuanzia leo Februari 15, 2020 ninajivua Ubunge wangu na nafasi zote za uongozi ndani ya CHADEMA, na nimeamua kujiunga na CCM' - Cecil Mwambe aliyekuwa Mbunge wa Ndanda

Tazama video kamili hapo chini