CHADEMA 'wacharuka' kuhusu Mange Kimambi

Thursday , 12th Oct , 2017

Mbunge wa Tarime Vijijini , John Heche amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Simon Sirro kutangaza kiama kwa wahalifu wa wanaofanya mauaji  kwa kupiga watu risasi siyo na siyo kuwatangazia wakosoaji wa Serikali.

Heche amelazimika kusema hayo baada ya hivi karibuni IGP Sirro alipokuwa mkoani Iringa kusema kwamba anafahamu makosa ya mtandaoni yanayofanywa na Mange Kimambi na kuahidi kwamba watamshughulikia.

"IGP anapaswa kuwatangazia kiama wahalifu na watu wanaofanya vitendo vya kupiga watu risasi& kutupa wengine baharini sio wakosoaji wa serikali"

Aidha Kiongozi mwingine wa Chadema aliyeingilia kauli ya IGP Sirro kuhusu Mange Kimambi ni Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema ambaye yeye alsema, 

"IGPSirro shughulika na usalama wa  raia, malizia uchunguzi BenSanane, TunduLissu na maiti zinazookotwa baharini. Achana na Mange Kimambi"

Hivi karibuni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Nyakoro Sirro alisema kuwa jeshi la polisi linatambua makosa ya kimtandao yanayofanywa na mwanadada Mtanzania Mange Kimambi aishiye nchini Marekani na kusema kuwa jeshi la polisi linashughulikia suala hilo.