Jumatatu , 15th Oct , 2018

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dkt. Vincent Mashinji wametofautiana kwenye kikao cha Kamati Kuu.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema amesema leo Oktoba 15, 2018 kwamba hakuna kikao chochote cha Kamati Kuu ambacho kimefanyika mwishoni mwa wiki hii, si tu nyumbani kwa mwenyekiti Mbowe bali popote pale.

"Tunaomba Watanzania na wanachama wetu wapuuze taarifa hiyo potofu inayosambazwa kwenye mitandao, tunaomba watanzania na Wanachama wetu wapuuze taarifa hiyo potofu inayosambazwa kwenye mitandao", imesema taarifa iliyotolewa na Mrema.

Amesema pia haijawahi kutokea wakati wowote vikao vya kamati kuu vikafanyika nyumbani kwa mwenyekiti wa taifa wa chama hicho kama ambavyo taarifa hizo zinadai.

Siku za hivi karibuni CHADEMA imekumbwa na wimbi la hamahama ya wabunge wake na kujiunga na CCM, huku sababu kuu inayotajwa na viongozi hao wanaojiuzulu ni migogoro ndani ya chama hicho inayosababishwa na mwenyekiti Freeman Mbowe.