CHADEMA waitikia wito polisi

Monday , 11th Sep , 2017

Viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo Septemba 11, 2017 kimeitikia wito wa jeshi la polisi kwa baadhi ya viongozi wake wakuu kufika makao Makuu ya jeshi hilo la Polisi jijini Dar es Salaam kufuatia sakata la Tundu Lissu.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Kwa mujibu wa habari iliyotolewa na CHADEMA imesema kuwa viongozi ambao wamefika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi ni pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Vicent Mashinji 

"Katibu Mkuu wa Chama Dkt. Vincent Mashinji, akiambatana na wasaidizi wake kutoka Makao Makuu ya Chama, mchana huu, amewasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam, kuitikia wito wa Jeshi la Polisi uliotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto, kuwa anatakiwa kufika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)" ilisema taarifa ya CHADEMA.