Ijumaa , 16th Aug , 2019

Rais wa Afrika ya Kusini Cyril Ramaphosa leo Agosti 16, ametembelea eneo la Mazimbu mkoani Morogoro, eneo ambalo linaonesha uhusiano mkubwa wa kihistoria kati ya nchi za Tanzania na Afrika Kusini.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Eneo hilo ndilo lililotumika kuwekea mijadala ya kupinga vuguvugu la ubaguzi wa rangi  katika nchi ya Afrika Kusini.

Akizungumza katika sehemu ya hotuba yake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mahusiano ya kihistoria kati ya Tanzania na Afrika ya Kusini yameendelea kushamiri kutoka na utangulizi wa viongozi walioweka misingi imara ya kuzuia ubaguzi wa rangi kwa nchi za Afrika.

''Changamoto zinazoikabili Tanzania katika nyanja mbalimbali zinafanana sana kwa kiasi kikubwa na changamoto ambazo ziko Afrika Kusini. Hii ni kutokana na historia yetu ya kijiografia kwa maana watu wa Afrika Kusini ni wale watanzania wote waliowahi kukutana na changamoto ya ubaguzi wa rangi na kutothaminiwa utu wao dhidi ya wakoloni'', amesema Waziri Mkuu

Katika ziara yake mkoani humo, Rais Ramaphosa atatembelea katika vyumba mbalimbali na kukiona chumba cha kwanza kilichotumika  kufanya mijadala kabla ya kwenda nchini Afrika Kusini  kupambana, pia ametembelea makaburi  ya mashujaa walioenda kupigania haki ya ubaguzi wa rangi na kupanda mti kama kumbukumbu katika eneo hilo.