Alhamisi , 2nd Apr , 2020

Chama cha Madaktari nchini (MAT), kimeiomba Serikali kuongeza vifaa vya kuwakinga watoa huduma za afya wanapowahudumia waathirika wa Virusi vya Corona pamoja na kutoa dawa za muda mrefu kwa wagonjwa, wanaochukua dawa kila mwezi ili kupunguza msongamano katika hospitali mbalimbali.

Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dkt Elisha Osati

Ombi hilo limetolewa leo Aprili 2, 2020 na Rais wa MAT, Dkt Elisha Osati, alipozungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, na kupongeza juhudi zinazochukuliwa na Serikali dhidi ya ugonjwa unaosababishwa na Virusi vya Corona.

"Ili watumishi wa Afya na Madaktari waweze kufanya kazi vizuri, tunahitaji pia kulindwa, tunahitaji vifaa vya kuweza kupambana na Corona kama Mask,ziendelee kupatikana, tuombe hata viwanda visaidie kutengeneza hivi vifaa ili waweze kuwalinda wananchi na watumishi wa sekta ya afya" amesema Rais wa MAT.