Jumapili , 24th Mar , 2019

Katibu Mkuu mpya wa Chama Cha Wananchi CUF, Khalifa Suleiman Khalifa amesema katika kipindi cha uongozi wake atahitaji kushirikiana kwa karibu na viongozi wa vyama vyote wakiwemo wa Chama Cha Mapinduzi ili kutimiza majukumu yake.

Akizungumza na www.eatv.tv Khalifa amesema katika kuhakikisha CUF mpya inazaliwa ni mpango wake anashirikiana na baadhi ya viongozi wenzake wa vyama vya upinzani pamoja na Chama Cha Mapinduzi.

Khalifa amesema kuwa, "nikikutana na kiongozi wa CCM, nitamwambia chama ni taasisi ambayo inadhamira ya kujenga nchi yetu, naomba tushirikiane na tusaidiane, ili tuapte mafanikio ya vyama vyetu".

"Ninaposema ushirikiano sisemi mimi nitachukua ilani yao nikaitekeleza, napokutana na Bashiru kwanini nigombane naye nikitengeneza ugomvi na Bashiru nitafaidika nini yeye ni Katibu Mkuu wa chama tawala sasa usipozungumza naye vizuri na viongozi wa CCM, unadhani utafanya mkutano wa hadhara", ameongeza Khalifa Suleiman.

Khalifa Suleimani ni Katibu Mkuu wa pili tangu kuanzishwa kwa Chama Cha Wananchi CUF, ambaye amerithi nafasi ya Maalim Seif Sharif Hamad ambaye alitangaza kuhamia Chama Cha ACT-Wazalendo baada ya mgogoro wa kiuongozi uliodumu kwa zaidi ya miezi miaka 3.

Hivi karibuni akizungumza na www.eatv.tv Katibu Mkuu Khalifa huyo alibainisha chama hicho hakitashiriki kwenye Umoja wa Katiba ya Wnanchi UKAWA, kwa kile alichokidai kutokuwepo kwa usawa.