Jumatano , 18th Jul , 2018

Mwanafunzi aliyekuwa Dada Mkuu katika shule ya sekondari ya Jangwani jijini Dar es salaam Mida Twaha Jumbe ameeleza moja ya sababu za Shule hiyo kupata matokeo mabovu ya kidato cha sita mwaka 2018 kuwa ni kuwepo ushirikiano hafifu kati ya wanafunzi na walimu.

Pichani ni wanafunzi wa Shule ya sekondari Jangwani wakiwa katika mwonekano wa furaha.

Akizungumza na www.eatv.tv Maida amesema kuwa wanafunzi siyo wa kulaumiwa pekee ila sababu za shule hiyo kuwa miongoni mwa shule kumi zilizoshika mkia ni mawasiliano haba kati ya wanafunzi na walimu, umbali kwa wanafunzi wanaoishi nje ya shule ikiwemo mahusiano ya kimapenzi kati ya wafanyakazi wa shuleni hapo na wanafunzi.

“Hakuna mwanafunzi ambaye anataka kufeli masomo na hakuna aliyefurahia matokeo haya maana wanafunzi wengi matokeo yao ya kidato cha nne wamepata division one, two na mzizi wa tatizo ni mfumo wa uongozi wa shule ambao haupo karibu na wanafunzi,” amesema Maida.

Aidha Maida ameongeza kuwa Wizara ya Elimu inapaswa kufuatilia mwenenendo wa uongozi wa shule hiyo na walimu wanapaswa kuwa karibu na wanafunzi kwa matokeo chanya pia walimu kuheshimu kazi yao.

Hatahivyo Maida amekanusha uvumi wa watu kuwa kuvaa sketi fupi au uwepo wa utandawazi hasa kuwepo vifaa kama simu, kompyuta siyo chanzo cha kufeli maana shule zilizofanya vizuri kama kibaha wanatumia vifaa hivyo.