Alhamisi , 22nd Aug , 2019

Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Christopher Ngumbiagai, amekiri kuongezeka kwa idadi kubwa ya wanafunzi katika Wilaya hiyo, ambao wamekuwa wakiacha masomo kutokana na mimba, huku watuhumiwa wakubwa wakiwa ni walimu na bodaboda.

Ngumbiagai ametoa kauli hiyo baada ya kupokea taarifa juu ya kusitisha masomo, kwa mwanafunzi wa darasa la 3, katika shule ya Msingi Nambondo wilayani Kilwa.

Ngumbiagai amesema licha ya juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali kuhusu suala la elimu, bado kuna changamoto hususani kwa wazazi ambao wamekuwa wakiyakalia kimya matukio hayo.

"Inasikitikisha sana licha ya Serikali kupambana kudhibiti mimba mashuleni ila tunarudishwa nyuma, na wanaotajwa kuongoza kuwapa mimba wanafunzi ambao ni walimu na madereva bodaboda" amesema Ngumbiagai.