Ijumaa , 19th Apr , 2019

Mwenyekiti wa Umoja wa Madiwani Kanda ya Serengeti kupitia CHADEMA, Emmanuel Ntobi,  amehoji suala la kuitwa kwenye Kamati ya Maadili ikiwa ni baada ya kuibua  ufisadi unaofanywa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga.

Rais Magufuli

Ntobi ambaye ni Diwani wa Kata ya Ngokolo ameitwa kwenye Kamati ya Maadili ya Madiwani kutokana na taarifa alizozitoa mitandaoni ambazo zinahusisha ufisadi wa mamilioni kwenye ujenzi wa machinjio ya kisasa, ujenzi wa kituo cha afya na mradi wa viwanja katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Katika taarifa nyingine, Ntobi anadai kuwa Mkurugenzi aligoma kumlipa mkandarasi shilingi milioni 6 lakini kwa haraka sana Halmashauri ikalipa milioni 55 ambazo zilitoka kwenye akaunti ambayo Madiwani walikubaliana isiguswe.

Katika ukurasa wake Ntobi amesema kwamba, "Mhe Rais  Magufuli nipo tayari kutoa ushahidi wa ufisadi TAKUKURU ama chombo chochote. Lengo la Mkurugenzi ni kunifungia vikao si kushughulikia ufisadi".

Kikao hicho cha Maadili pamoja na Diwani Ntobi kinatarajiwa kufanyika tarehe 23 Aprili mwaka huu.