
Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson
Dkt. Tulia amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua mafunzo ya umoja wa wabunge wanawake kutoka nchi za jumuiya ya madola ambayo yanalenga kuwajengea uwezo wabunge hao namna ya kuongeza wabunge wanawake kwenye mabunge ya nchi wanazotoka.
Akizungumza katika mafunzo hayo Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima, amesema kuelekea kwenye jukwaa la usawa wa kijinsia Tanzania imekuwa ikifanya vizuri hivyo kupitia majukwaa hayo wanawake watahamasishwa kushiriki kwenye nyadhifa za uongozi kwa kuwezeshwa kupitia majukwaa hayo.