Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka.
Mtaka ameyasema hayo wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo cha Polisi Chang’ombe, ambacho kukamilika kwake kutaondosha adha ya matendo ya uhalifu ikiwemo ukabaji, uporaji na matendo ya udhalilishaji.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde amesema matendo ya uhalifu yamekithiri na wanaishukuru Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kuona haja ya uwepo wa kituo katika eneo hilo.
Tazama video hapa chini