'Eti Mkuu na huku, nitafyeka vichwa vyenu' -Mwanri

Ijumaa , 17th Jan , 2020

Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri, amesema hana mpango wa kuwavumilia baadhi ya  Maafisa watendaji wa Mitaa wazembe, waliopo katika Manisipaa ya Tabora.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri.

RC Mwanri amesema kuwa amejipanga kuwatimua hii ni kutokana na wao kushindwa kutambua wajibu wao, ikiwemo kutosimamia na kudhibiti uharibifu wa mazingira na miundombinu yake, ambao umekuwa ukifanywa na wananchi ndani ya Mji huo.

"Imefikia hatua mmepauka 'you have got no modal authority' ya kusimama mbele ya watu na kuwaambia hili jambo haliwezekani, mnabaki tu kuagiza Mkuu njoo na huku bwana, hakuna cha Mkuu njoo na huku bwana, wote nafyeka vichwa vyao" amesema RC Mwanri.

Aidha RC Mwanri amesema hakubaliani na hali ya watendaji hao kushindwa kuwa na namna  nzuri ya kutatua kero ndogondogo za wananchi, mpaka aitwe Mkuu wa Mkoa.