EXCLUSIVE: Mke wa Kigwangalla amzungumzia Mumewe

Jumapili , 12th Jul , 2020

Mke wa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamis Kigwangalla, Dkt Bayoum Awadhi, ameeleza ni kwa namna gani huwa ana-miss uwepo wa mume wake nyumbani hii ni kutokana na Dkt Kigwangalla kuwa na majukumu mengi ya kikazi yanayopelekea kutokuwepo nyumbani kwa wakati.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamis Kigwangalla na Mke wake Dkt Bayoum.

Dkt Bayoum ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na EATV, mara baada ya kuulizwa ni changamoto gani anayokumbana nayo kuwa na mume ambaye ni kiongozi na anakimbizana na mikiki ya huku na kule na kuongeza kuwa yeye huwa anajitahidi kuliziba pengo la mume wake kwa watoto wao ili na wao wasijisikie wapweke, pindi Baba yao anapokuwa hayupo nyumbani.

"Changamoto ziko nyingi, lakini kubwa ni kum-miss nyumbani tunatamani kuwa naye, sana nawaonea hurumia watoto, 'Sometime i try to fill the gap' ili kuwafanya watoto waone hakuna shida Baba yupo, lakini kadiri siku zinavyozidi nazidi kujifunza na kuzoea namshukuru Mungu ameniwezesha" amesema Mke wa Dkt Kigwangalla.

Tazama video hapa chini.