Alhamisi , 22nd Aug , 2019

Katibu mkuu wa umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi kitaifa, Mwalimu Reymond Mangwala, ameagiza kufanyika matembezi ya umbali mrefu yatakayohusisha vijana kote nchini wakielekea kijijini Mwitongo alipozaliwa Baba wa taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Msemaji wa familia ya Mwalimu Nyerere, Chief Wanzagi

Mwangwala amesema hayo wakati akizungumza na vijana, katika kongamano la Tarime ya kijani, liliyofanyika wilayani Tarime mkoani Mara.

Kwa upande wake Msemaji wa familia ya Mwalimu Nyerere, Chief Wanzagi, akiwa kijijini Mwitongo wilayani Butiama, amesema Jamii pamoja na viongozi wa serikali wanajitahidi kumuenzi Mwalimu kwa vitendo.

''Kwa ujumla viongozi wanajitahidi kuyaenzi na kuyafuata mawazo ya mwalimu, hata viongozi wa awamu ya sasa wanafanya mambo kwa kumtaja yeye katika kile eneo na wanatuongoza katika kumuenzi'', amesema Chief Wanzagi.

Matembezi hayo ya umbali mrefu yanalenga kumuenzi na kudumisha fikra zake, ikiwemo vita dhidi ya Rushwa na ukabila wakati tukielekea kuadhimisha miaka 20 tangu kifo cha Mwalimu Nyerere.