Jumanne , 16th Oct , 2018

Mwanasheria maarufu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Fatma Karume, amefunguka juu ya vitu ambavyo yeye hupenda kuvifanya kwa mume wake kama ilivyo kawaida kwa wanawake wengi wa Pwani.

Rais wa chama cha wanasheria Tanganyika, Fatuma Karume.

Akipiga stori na 'Big Chawa' kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Fatma Karume amesema kuwa yeye kama mwanamke wa Kizanzibari, hupenda kupaka hina kama urembo ili kumfurahisha mume wake.

Hina Wazanzibari tunapaka sikukuu, Eid, mume wangu akirudi safari huwa napaka, sasa itabidi umwambie mume wangu asafiri ili nipake”, amesema Fatma Karume huku akicheka.

Fatma ameendelea kutoa siri kwamba mara nyingi huwa anakuwa na mume wake pale anapopata fursa ya kupumzika, na kutoka naye sehemu mbalimbali za starehe ili kujifurahisha.

Licha ya kutotaka kumtaja mume wake huyo, Fatma Karume amesema pia kuwa mume wake huwa anapenda kumuimbia wanapokuwa wawili, au wakiwa kwenye gari wakielekea sehemu mbali mbali.