"Haiwezekani kuiangusha CCM" - Nape Nnauye

Ijumaa , 12th Jan , 2018

Mbunge wa jimbo la Mtama, Mhe. Nape Nnauye amefunguka na kusema upinzani nchini Tanzania hautaweza hata siku moja kukiangusha Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika madaraka kwa kuwa inapofika wakati wa kutafuta dola hawana urafiki na mtu. 

Nape Nnauye amesema hayo alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombe ubunge wa jimbo la Longido kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi ambao unatarajiwa kufanyika kesho Januari 13, 2018.  

"Ikifika wakati wa kutafuta dola CCM inakuwa kitu kingine kabisa, unaweza kuichezea wakati wa kawaida na tunaweza kupiga stori ila ikifika kwenye kutafuta dola hapo ni mambo mengine kabisa. Ndiyo maana nasema wenzetu watasubiri sana kwani haiwezekani kuiangusha CCM madarakani" alisisitiza Nape Nnauye