'Hakuna Ibada ya Eid Kitaifa' - BAKWATA

Jumapili , 17th Mei , 2020

Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA), limeeleza hakutakuwa na Swala ia Eid ya Kitaifa wala Baraza la Eid na kuwataka waumini wake kufanya ibada kwenye misikiti yao ya karibu kwa kufuata taratibu za afya, ikiwa ni hatua ya kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona.

Mufti Mkuu wa Tanzania Aboubakari Zuberi

Kupitia barua iliyotolewa na Katibu Mkuu wa BAKWATA, Nuhu Jabir Mruma imesema utaratibu wa kusherehekea sikukuu hiyo ya Eid itatangazwa hivi karibuni na Baraza hilo.

Imesema sikukuu hiyo ya Eid huenda ikaangukia siku ya Mei 24, au Mei 25 kutegemeana na muandamo wa mwezi huku ikiwatakia sherehe njema waislamu wote.