Jumatatu , 10th Aug , 2020

Mwenyekiti wa Chama cha CHAUMA Hashim Rungwe, leo Agosti 10, 2020, amechukua fomu ya kuwania Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwezi Oktoba katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), zilizopo Dodoma.

Mgombea Urais kupitia CHAUMA Hashim Rungwe akiwa na mgombea mwenza Mohammed Masoud.

Rungwe amefika katika ofisi hizo mapema leo asubuhi akiongozana na mgombea mwenza Mohammed Masoud, na kukabidhiwa fomu hizo na Mwenyekiti wa NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage.

Mgombea Urais pia wa chama cha CUF Profesa Ibrahim Lipumba, kesho Agosti 11, atawasili kwenye ofisi za NEC kwa ajili ya kuchukua fomu hizo. 

Zoezi la kuchukua fomu hizo litahitimishwa Agosti 25, 2020, ambapo mpaka sasa vyama ambavyo tayari vimekwishachukua fomu ni pamoja na CCM, CHADEMA, ACT WAZALENDO, SAU, ADC, UPDP, NRA, AAFP pamoja na DP.