Hatma ya kigogo CHADEMA aliyekataa mil 200 za CCM

Jumatano , 5th Dec , 2018

Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa imehairisha kesi inayomkabili, Meya wa Manispaa ya Iringa Mjini, Allex Kimbe dhidi ya tuhumza ya kupokea rushwa ya milioni 2 na kukamatwa inayomkabili.

Meya wa Manispaa ya Iringa Mjini, Allex Kimbe.

Kesi hiyo ya Meya wa CHADEMA ilipangwa kuanza kusikilizwa leo na mahakama hiyo lakini imeahirishwa baada ya upande wa Jamhuri kueleza kuwa haujakamilisha ushahidi ambapo imepangwa kusikilizwa tena Disemba 20 mwaka huu.

Asubuhi ya Novemba 16, 2018 kulisambaa taarifa kuwa Meya huyo wa Iringa Mjini, alikamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kwa madai ya kukutwa na fedha ya mtego zaidi ya shilingi milioni 2 za mzabuni, Nancy Nyarus.

Akizungumza na www.eatv.tv Meya Kimbe alitoa madai ya kuwa amekuwa akijikuta na kesi nyingi mahakamani kwa kile alichokidai kuwa alizikataa milioni 200 za chama hicho ili ajiunge nao.

"Wanafanya yote hayo ili nikubali milioni 200, nijiunge nao na mara ya mwisho walinifuata baadhi ya viongozi wa CCM ili wanipatie hizo fedha na wanifutie kesi, na huu msimamo wangu ndiyo chanzo kikubwa haya yote," alisema.