
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Bashiru Ally.
Bashiru Ally ametoa kauli hiyo wakati akiwa mkoani Kagera ambapo amesema maelekezo hayo ni kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa ambapo amesema wamejipanga kutumia gharama ndogo kwenye Uchaguzi ujao.
Bashiru Ally amesema kuwa "matarajio yangu uchaguzi ujao tutatumia pesa kidogo, na tumeshasema hatutanunua tisheti za kuwagaiwa wanachama wakati wa Uchaguzi"
"Hakuna cha burena kwakweli hakuna cha bure kama Makao Makuu wanachapisha tisheti kuwapa wanachama maanake wamewaomba kwa Matajiri" amesema Bashiru Ally