Jumapili , 20th Sep , 2020

Jengo la ofisi kuu la chuo kikuu cha Makerere Ivory Tower nchini Uganda limeungua moto usiku wa jana ambapo mpaka sasa chanzo cha moto huo hakijajulikana.

Jengo la Ofisi Kuu la Chuo Kikuu cha Makerere 'Ivory Tower'

Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini humo, tangu kuzuka kwa moto huo usiku wa jana hakijaripotiwa  kifo au majeruhi yoyote isipokuwa uharibifu wa mali ambazo zilikuwa ndani ya jengo.

Jengo hilo lenye takribani miaka 79 lilifanikiwa kuokolewa kutokana na moto huo ambapo ilibainika baadhi ya vitu ambavyo vilivyokuwa ndani ya ofisi hiyo vimeteketea.

Ujenzi wa jengo hilo ulikamilika mwaka 1941 chini ya uongozi wa Mkuu wa Chuo, George C. Turner. Jengo hilo kuu ni moja ya kivutio kikubwa katika Jiji la Kampala, kutokana na muonekano wake kufanana na majengo ya Kiingereza.