Jumatano , 15th Aug , 2018

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, leo Agosti 15, 2018 amefanya mabadiliko madogo kwa kuwahamisha makamanda wa Polisi katika mikoa ya Mwanza na Pwani.

IGP Simon Sirro

Katika mabadiliko hayo IGP Sirro, amemuondoa aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Kamishna msaidizi wa Polisi (DCP) Ahmed Msangi na kumhamishia makao makuu ya upelelezi Dar es salaam kuwa mkuu wa kitengo cha makosa dhidi ya Binadamu.

Nafasi yake imechukuliwa na Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shana aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani.

Aliyekuwa RPC wa Mwanza Ahmed Msangi.

Kwa upande mwingine Sirro amemteua Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Wankyo Nyigesa ambaye alikuwa Mkuu wa Operesheni kanda maalum ya Dar es salaam kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani akichukua nafasi ya Jonathan Shana.

Taarifa ya Jeshi la Polisi imeeleza kuwa mabadiliko haya ni kawaida na yanalenga kuongeza ufanisi na utendaji kazi ndani ya jeshi hilo.