Alhamisi , 12th Jul , 2018

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewaomba Viongozi wa dini nchini kuendelea kufanya doria za kiroho huku Jeshi hilo likiendeleza doria za kimwili kwa pamoja ili kuukabili uhalifu ikiwemo mauaji yanayosababishwa na wivu wa mapenzi yaliyoshamiri siku za hivi karibuni.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akiwasalimu viongozi wa dini.

IGP Sirro ameyasema hayo katika  Wilaya za Ukerewe na Sengerema mkoani Mwanza wakati wa Ziara yake inayoendelea katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa yenye lengo la kubaini changamoto za kiuhalifu na kuzipatia ufumbuzi wa haraka ili wananchi waendelee kufanya kazi zao kwa Amani na utulivu.

Polisi tunafanya kazi zetu ambazo wakati mwingine hutumia nguvu kushurutisha watu kutii sheria lakini Viongozi wa dini pia mna nafasi yenu katika jamii kwa kukemea maovu”, amesema Sirro.

Katika hatua nyingine IGP Sirro ameahidi kuchangia Shilingi milioni kumi na tano ili kusaidia ujenzi wa kituo cha Polisi katika Kisiwa cha Kome, Wilayani Sengerema baada ya Wananchi kuomba kujengewa kituo hicho ili kukabiliana na uhalifu.