Jumatatu , 21st Mei , 2018

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limetoa onyo kwa wazazi na walezi wanaowafanyia watoto vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuwajeruhi ama kuwatelekeza na kuwafanya watoto hao kuishi katika mazingira hatarishi kuacha mara moja kwani wanachokifanya ni kosa kisheria.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoano Mwanza Ahmed Msangi wakati akifanya mahojiano na eatv.tv leo Mei 21, 2018 na kusema vipo vifungu vya sheria vinavyowapa mamlaka Jeshi la Polisi kuwakamata watu wanaowatendea ndivyo sivyo watoto kwa makusudi.

"Wazazi wanapaswa kuwalea vizuri watoto wao na kuacha tabia ya kuwanyanyasa na kuwatelekeza. Tutatumia hizo sheria ili kuhakikisha watoto wanatunzwa vizuri na kuepuka kuwa na majambazi baadae katika miaka inayokuja", amesema Msangi.

Mbali na hilo, Kamanda Msangi amesema endapo itatokea mzazi atakaebisha kufanya hivyo kwa makusudi basi atakamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa mujibu wa sheria.

Msikilize hapa chini Kamanda Ahmed Msangi akielezea zaidi...