Jumanne , 17th Apr , 2018

Wazazi wawili wenye dini ya Kiislam nchini Ufaransa wamepelekwa mahakamani baada ya kumpa mtoto wao jina la 'Jihad' na kujaribu kulisajili rasmi serikalini.

Picha sio ya watu husika (kwa hisani ya mtandao)

Maafisa wa serikali wa Ufaransa baada ya taarifa hiyo waliamua kuwafikisha kwa waendesha mashtaka, ambao sasa hivi wanaendesha kesi hiyo kupingana nalo wakiamini kuwa jina hilo lina muunganiko na ugaidi.

Wazazi hao walijaribu kujitetea kwa kuwaeleza waendesha mashtaka kwamba jina hilo halina maana ya vita vitakatifu kama ambavyo wengi wanafahamu, bali ni nguvu na kuweza kujipigania.

Hata hivyo maafisa wa serikali wa Ufaransa wamesema wamewataka wazazi hao kubadili jina la mtoto huyo ili kumlinda na madhara yake baadaye, na wazazi hao kufikia muafaka hapo jana April 16, 2018, na kumuita Jahid.

Nchini Ufaransa mzazi ana uhuru wa kumpa mtoto jina lolote analopenda, lakini lisiwe na madhara kwenye maisha ya mtoto huyo kwa namna yoyote ile.