Jumatano , 19th Sep , 2018

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo, amebainsha changamoto 6 ambazo anahitaji kupambana nazo ili kuinua kiwango cha ufaulu wa elimu katika wilaya ya kisarawe kuanzia elimu ya Msingi mpaka kidato cha sita.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari wilayani kisarawe Mkoani Pwani Dc Jokate amesema wilaya hiyo inahitaji shilingi bilioni 4.1 ili kumaliza changamoto za elimu wilayani kisarawe.

Changamoto hizo ni?

MADAWATI 1166

Changamoto ya mdawati katika wilayani kisarawe ni miongoni mwa matatizo ambayo mkuu huyo wa wilaya ameahidi kuifanyia kazi ambapo wilaya hiyo inauhitaji wamadawati 1166 ambapo kwa sekondari uhitaji ni 484, na 642
kwa shule ya msingi na gharama yake  ni milioni67.

MATUNDU YA VYOO 113

Jokate pia amebaisha wilaya hiyo inahitaji zaidi ya shilingi milioni 124 kwa ajili ya kujenga matundu ya vyoo 113 kwa shule za wilaya hiyo.

OFISI ZA WALIMU

Wilaya hiyo pia inauhitaji wa ofisi za walimu za kisasa katika shule 14 ambazo zinagharimu shilingi milioni 880.

MAKTABA 13

Jokate alisema wilaya hiyo pia inauhitaji wa maktaba za kujisomea na wanafunzi wajifunze zaidi.

“..Katika kutokomeza zero wilayani Kisarawe, mwaka huu tumejipa mtihani wa kuwashirikisha wadau ili kutatua changamoto za miundombinu itakayowezesha kuinua ufaulu wa elimu kisarawe.”

Changamoto zingine ni VYUMBA VYA KULALA WANAFUNZI (HOSTELI), MAABARA ZA KISAYANSI,

Pia katika hatua nyingine, Mh. Jokate  amesema msaada wa usafiri (Lifti) unaotolewa na Madereva wa bodaboda kwa wanafunzi wakike katika shule zilizopo wilayani Kisarawe zimetajwa kuwa ni miongoni mwa changamoto zinazowafanya wanafunzi wa kike kukumbwa na vishawishi viovu.

Kwa mujibu Mkuu Wilaya ya Kisarwe msaada wa usafiri "lifti" zinazo tolewa na madereva bodaboda kwa wanafunzi wamegundua kuwa madereva wanatumia nafasi hiyo kuwalaghai wanafunzi wakike huku akiwataka bodaboda kuwa mabalozi wakuwalinda wanafunzi wakike ili kumaliza masomo yao.

Mkuu wa wilaya Jokate amesema "...tumekua na kesi nyingi sana kwa bodaboda, wakiwapandisha watoto wakike lift na wao humohumo wanaingiza ajenda zao, tumegundua na wao wanachangia kupotosha watoto wakike kusoma,."