Jumapili , 5th Jul , 2020

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo amemtaka Mkurugenzi kuweka mazingira mazuri ikiwemo kupunguza bei ya maeneo ili kutoa fursa kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza ndani ya wilaya hiyo waweze kumudu gharama.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo

Jokate ameyasema hayo katika kikao cha Baraza la Wafanyabiashara wilayani humo, baada ya Afisa Biashara wa Halmashauri ya Kisarawe Joachim Costa kuwasilisha ripoti ya biashara ikionyesha zaidi ya biashara 180 zenye thamani ya shilingi milioni 9 na laki 3 zimefungwa wilayani Kisarawe katika kipindi cha kuanzia mwaka 2019 hadi 2020.

''Tutajitoa kushirkiana na wafanyabishara na wawekezaji wetu, mtu akija hapa hahitaji kukuta vizingiti vingi vya yeye kufanya uwekezaji, hivyo Mkurugenzi angalia maeneo mengine ambayo mtu atatumia gharama za chini kabisa kwasababu lengo letu ni kuvutia wawekezaji'', amesema Jokate.

Aidha Afisa Biashara alibainisha kuwa sababu za biashara hizo kufungwa ni wateja kushindwa kumudu gharama kwenye bidhaa zinazozalishwa Kisarawe pamoja na kuvunjwa kwa miundombinu kwaajili ya kupisha upanuzi wa barabara hali inayopelekea kuathiri biashara nyingi wilayani humo.
 

Tazama Video hapo chini